Mimi Mars Afungukia Furaha Aliyonayo Kutokana na Kuwa Single

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachompa furaha kama kuwa single kwa sababu yupo huru kufanya kazi zake vizuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Showbiz, Mimi Mars alisema, aliamua kuishi peke yake bila mwanaume kwa sababu ameshawahi kuumizwa na aliokuwa akiwapenda hivyo kumfanya kuwa mpweke na kushindwa kufanya kazi zake vizuri.

download latest music    

Niliishia kuambulia maumivu tu kutokana na kuwa na wanaume wasiokuwa waaminifu, nikaona hapana, kwa nini niendelee kuteseka wakati kuna maisha baada ya mapenzi? Hivyo nimeamua kuishi mwenyewe mpaka pale nitakapompata mtu sahihi, nayafurahia haya maisha kwa sasa”.

Mimi Mars ameshawahi kutajwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Staa wa muziki wa hip hop nchini Kutokea katika Kundi la Weusi Joh Makini.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.