Mimi Mars Akanusha Tetesi za Mahusiano ya Kimapenzi na Joh Makini

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mdee Music Mimi Mars, amekanusha tetesi zinazosambaa juu yake kuhusu mahusiano yake na  msanii mwenzie Joh Makini.Mimi Mars amesema kuwa watu wamekuwa wakizusha kuwa anatoka kimapenzi na joh makini  bila kujua kuwa yeye na joh makini ni kama kaka yake kwa sababu wamekuwa wanamuona akiwa rafiki ya kaka yake.

Mahusiano yangu   na Joh Makini ni ya kikaka na dada,kwa sababu Joh Makini  ni mtu ambae tumekuwa tunamjua kutokana na ukaribu wa kirafiki na kaka yetu mkubwa.Alikuwa rafiki yake mkubwa na kaka yetu kwaio kama vile ambavyo kaka yetu amekuwa wakitushauri ndivyo Joh Makini  anafanya, kwaio ni kaka na ni mshauri hayo maswla ya mahusiano sijui yametokea wapi.

Lakini pia Mimi Mars anawasema kuwa watu wanatakiwa kuwa wanaongea yale wanayokuwa na uhakika nayo kwa sababu mara nyingine inaweza kuahribu mahusiano ya watu bila wao kujua kuwa maneno yasiyokuwa na ushahidi yanaweza kubomoa kabisa.Mimi Mars anasema kuwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mtu yoyote.

download latest music    

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.