Mimi na Esma Muda Wote Tukikutana Tunapiga Umbea Tu;-Queen Darleen

Mwanadada mrembo pekee kutoka WCB amefunguka akiwa anaongea na dizzim online na kutoa msimamo wa mahusiano yake na dada yake ambae ni Esma Platinumz na kukanusha kuwa hawana mahusiano mazuri kama watu wanavyodai katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na mwandishi Queen anasema kuwa yeye na Esma mara nyingi wakikutana wanapiga sana umbea kuhusu mambo ya mjini na wanaongea vizuri kama kawaida”mimi na esma wambea haswa, tukikutana muda wote sisi tunazungumzia vitu vya umbea tu. kwanza tukikaa na Esma dakika mbili lazima tugombane.”

download latest music    

Lakini pia Queen amezungumza kuhusu kutokuonekana kwa rich mavoko WCB na hata kutoa nyimbo kwa sasa na amesema “mavoko yupo na mavoko tunafanya nae kazi ofisini kama kawaida hakuna tatizo lolote lile.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.