Mimi na Hemed Tumekuwa Tukigombana kila Baada ya Wiki Mbili :-Gelly
Msanii anaetamba kwa sasa na wimbo wake wa Washa amefunguka na kuongelea mahusiano yake na msanii mwenzake Hemed ambae anasema kuwa walikuwa watu wa kugombana sana kipindi cha nyuma lakini kitu cha ajabu ni kwamba kwa sasa hivi wamekuwa marafiki sana.
Gelly anasema kuwa hata katika baadhi ya kugombana kwao ilikuwa ni kwa sababu ya wanawake ambapo anasema kuwa hemedi alikuwa anweza kumzidi kete na akamchukulia mademu zake na hivyo yeye anachofanya pia ni kukaa vizuri na kujipanga na kumchukulia pia.
Mimi na Hemed tumekuwa tukigombana na kuzozana kila baada ya wiki mbili,, tulishapigana sana lakini kwa sasa tumekuwa zaidi ya marafii yaani ni kama ndugu. Ananichukulia demu wangu na mimi nikikaa vizuri namchukulia wa kwake.
Kwa kumalizia katika mahojiano hayo Gelly anasema kuwa amekuwa mtu mwenye ndoto kubwa ya kutaka kuwa Producer wa filamu zenye mafanikio .