Mimi Ndio Mtu wa Kwanza Kupata Mtu wa Kunisaidia Ilipovunjika Ya Moto:-Beka

Msanii wa muziki anaefanya vizuri kwa sasa na  nyimbo zake mbalimbali Beka Fleva amefunguka na kusema kuwa nashukuru mungu sana kwa sababu  baada ya kuvunjika kwa ya moto yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kupata mtu wa kumsaidia kuendelea na muziki.

Beka anasema kuwa siku meneja wao  wa bendi anatangaza katika media kuwa kuanzia sasa wasanii wa band ya ya  moto watakuwa free kufanya muziki wao wenyewe alikuwa moja  ya watu waliokuwa na stress sana kwa sababu alikuwa keshazoea kuwa anafanyiwa kila kitu wao kazi yao kuimba tu , ukizingatia kuwa walikuwa hawajuani hata na watengenezaji wa muziki kwa sababu hawakulelewa hivyo katika band.

download latest music    

Akiongea katika Clouds 360, beka ansema kuwa baada ya kutoka katika interview siku hiyohiyo mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Silaji alimtafuta kwa simu na kumwambia kuwa anapenda sana muziki wake na anaomba kufanya nae kazi.

Beka anasema kuwa baada ya hapo alipewa ela ya kutoa wimbo wa Libebe na Sikinai na baada ya hapo alianza kupata ela kutoka katika show na kuanza kufanya mwenyewe lakini bado mtu yule aliyemsadia mpaka leo anafanya nae kazi na ndio amekuwa kama mkurugenzi wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.