“Mimi ni Bilionea” Zari Amwagia Povu Mange Kimambi

Zarinah Hassan au maarufu kama Zari The Bosslady ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amemwagia povu zito Mange Kimambi.

Mange na Zari wamerudi tena vitani huku safari hii Zari akiweka wazi kuwa yeye ni bilionea hivyo asimchukulie Poa.

download latest music    

Sakata hilo lilianza siku ya jana baada ya Zari kumwagia sifa marehemu Ivan za kuwa baba bora na sio mzazi mwenzake Diamond ambapo Mange alimjia juu na kumtaka amshukuru Diamond kwa sababu yeye na watoto wake wanaishi kwenye nyumba ya Diamond.

Baada ya Kuambiwa hivyo Zari alimwaga povu zito na kudai Mange ndio anaishi Kwenye makazi yasiyoeleweka nchini Marekani lakini yeye anaishi Kwenye nyumba ya Diamond kwa sababu ameamu.

Zari aliendelea kumwaga povu na kudai kuwa akiamia kuhaama anaweza kwa sababu Ivan ameacha nyumba tatu na yeye pia anamiliki nyumba moja na kusisitiza kuwa yeye ni bilionea.

Kama utakumbuka Mwanzoni mwa mapenzi yao Diamond alimnunulia Zari bonge la mjumba Nchini South Africa ambapo ndipo anaishi na Watoto wake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.