Mimi ni Mfanyabiashara Sitakiwa Kuchagua Upande Kati Ya Wasafi Au Clouds-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Abdul Chande Maarufu Kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni mfanyabiashara hivyo hawezi kufungamana na upende wowote.

Mgawanyiko huo kati ya wasanii ulitokea mapema Wiki iliyopita Baada ya sakata la Wasafi Festival na Fiesta lilopelekea wasanii waliokuwa wanaperfom kwenye Fiesta kushindwa kufanya hivyo na kuaababisha kukosa shoo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago TV, Dogo Janja ameweka wazi kuwa hawezi kujiweka katika upande wowote ule kwa sababu yeye ni mfanyabiashara hivyo kokote atakapoitwa kupiga pesa yeye ataona sawa tu.

Mimi matabaka sioni ninachoamini Mimi mfanyabiashara hivyo sitakiwa kufungamana na upande wowote ilimradi naenda huku napiga naenda kule napiga hela basi hicho cha maana kwangu”.

Dogo Janja alikuwa mmoja wa wasanii ambao walitakiwa kupiga shoo ya Fiesta jumamosi iliyopita lakini walishindwa Baada ya shoo hiyo kuhairishwa Baada ya serikali kuizuia kufanyika katika viwanja vya Leaders.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.