“Mimi sihitaji sifa za kijinga” Hamisa Mobeto aweka wazi ishu ya kupachikwa mimba na Diamond

Hamisa Mobeto amefunguka kuhusu madai kuwa msanii Diamond Platnumz ndo baba wa  mtoto anayembeba tumboni mwake.

Mrembo huyo aliweka wazi kuwa Diamond hakumpachika mimba, alisema hawezi tambua hadharani nani ndo baba wa mtoto wake mtarajiwa kwasababu hayo ni mambo yake ya kibinafsi.

download latest music    

“Huu uvumi unataka niweke wazi maisha yangu. Hilo halitajitokeza kwangu kwani mtu akishaumwa na nyoka akimuona mjusi anamuogopa. Baba wa mtoto wangu mtarajiwa namjua mimi na familia yangu. Nadhani inatosha.

“Sidhani kama ni lazima nimtaje kwenye media (vyombo vya habari) lakini wale wanaosema ni Diamond tafadhali sana, siye. Baba wa mtoto wangu yupo na sio matangazo ya biashara kila mtu majue mpenzi wangu.

“Hao wanaotutukana mbona maisha yao wameyaweka siri, au mimi tu ndiyo nijianike? Siwezi kufanya hivyo, najua nachokonolewa ili niseme lakini sitasema,” amesema Hamisa.

Hamisa pia alikana madai kuwa anatafuta kiki kwa kutumia jina la Diamond, alisema yeye haitaji sifa za kijinga.

“Maisha yangu binafsi yatabaki kuwa yangu mimi mwenyewe ila ya kibiashara yatajulikana na kila mtu. Mimi kwa sasa sihitaji sifa za kijinga, nahitaji mashabiki zangu wafahamu nafanya nini katika jamii na wanishabikie hivyo, sio kwa maisha yangu binafsi.

“Kuruhusu ushabiki katika maisha yako binafsi hasa ya mapenzi ni kujijengea uadui na marafiki wa uongo ambao wengi wao wanakuja kinafiki na kujifanya wanakufahamu kiundani au mpenzi wako kumbe ni waongo. Wanataka kuwavuruga na wakifanikiwa hutawaona,”alisema Hamisa.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere