“Mimi Sina Tatizo na Hamisa” Amefunguka Diamond Baada ya Mahakama Kuwasuluhisha

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya uhusiano wake na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya kumaliza tofauti zao mahakamani jana na Diamond kudai hana tatizo na Hamisa.

Siku ya jana tarehe 8 mwezi wa 2 Diamond na Hamisa walifika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza shauri la malezi ya mtoto wao anayejulikana kama Abdul Naseeb au Dylan.

download latest music    

Tangu mtoto huyu azaliwe kumekuwa na maneno mengi na tuhuma mbali mbali zikirushwa kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na Mama huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kuhusu malezi ya mtoto wao.

Baada ya kutoka mahakamani Diamond aliongelea kesi yao ilivyoenda na kuonyesha kufurahishwa na matokeo ya kesi hiyo ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv alifunguka yafuatayo:

Kila kitu kimeenda vizuri kwani tulichokuwa tunafanya ni kuwekana sawa ili kila mmoja ajue majukumu yake mimi kama Baba nijue nafanyaje na yeye kama mama hivyo hivyo, Alafu ile haikuwa ni kesi ndio maana unaona hatukuenda hata kizimbani tulikaa tu chini tukazungumza na kila mtu azungumze anataka nini yote ili tujue tunamleaje mtoto wetu katika malezi yaliyo bora.

Mnajua mkiwa na ugomvi kila mmoja anaongea lake kwaiyo leo tulikuwa tunawekana sawa ili tumlee mtoto wetu akue katika misingi iliyo bora, alafu hivi viasi vya pesa tunavyotaja mitandaoni mara oh mimi nataka milioni 10 tunakuwa tunazungumza tu lakini kiukweli mtoto anataka malezi mengi kuna wakati mwingine kama mwanao una uwezo wa kumpa hata milioni mia ila hautampa kwa sababu ulishaandikiwa milioni 10 hiyo haimsaidii mtoto lakini tumeweka mazingira mazuri na nimeweka kiasi kizuri ambacho kitaweza kumsaidia aweze kukua ni mtoto wangu na pia kwenye maisha kuna kupanda na kushuka”.

Diamond alipata kutaja kiasi alichopangiwa kutoa kwa mwezi na kusisitiza ni mambo ya kifamilia lakini pia ameongelea kumaliza tofauti zake na Hamisa na kusema kuwa yeye na Hamisa hawakuwa na bifu lolote bali kuna pande zilizokuwa zinawachochea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.