Miss Tanzania Afumaniwa Miezi Miwili Baada Ya Ndoa

Miss Tanzania mwaka 2008 Jackline Chuwa amepatwa na fedheha ya mwaka Baada ya kudaiwa   kufu­maniwa na Mume wake wa ndoa miezi miwili Baada ya kufunga ndoa.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti  kuwa, Chuwa alifumaniwa na mume wake Leonis Ngasa akiwa na mwanaume mwingine (jina halikupa­tikana mara moja) hivi karibuni wakati ndoa yao ikiwa ingali na miezi miwili tu na ushee.

download latest music    

Imedaiwa kuwa, tukio hilo limetokea maeneo ya Tabata Shule jijini Dar am­bapo shuhuda wa tukio hilo, alilitonya Ijumaa Wikienda kwamba baada ya kufumania, mume wa Jack (Ngasa) alijikuta ametupwa nyuma ya nondo Kituo cha Polisi Tabata-Shule kwa tuhuma za kumpa ‘vitasa’ mkewe

Baada ya sakata hilo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Miss Tanzania ili kupata ukweli Wake hii ya sakata hilo ambapo walitaka kujua kama yupo Muhimbili anapatiwa matibabu kama ilivyodaiwa ambapo alipokea simu na kudai kwamba hajafumaniwa lakini akasema amepata matatizo.

Hizo habari ni za uongo sijui hata mmezitoa wapi jamani kwanza mimi wala sipo Dar nipo Arusha na nina matatizo nimepata ajali kwa sasa nipo hospitali napatiwa matibabu sipendi kuchafuliwa na habari za uongo ja­mani“.

Mimi mwenyewe nimesikia tu yupo kituoni lakini sijajua kapatwa na nini, hilo gari ni langu ila mume wangu hajanifumania huo ni uongo, msiamini kila mnachosikia kwa watu jamani, wengine wana lengo la kunichafua tu mi’ sipendi kabisa hayo mambo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.