Miss Ubungo Awakumbuka Wanafunzi wa Umoja.

Aliyewahi kuwa Miss Ubungo mwaka 2014-2016 Diana Kato amewakumbuka wanafunzi wa shule ya umoja na kusherekea siku ya kunawa mikono Duniani pamoja shuleni hapo ikiwa kama moja ya njia ya kukumbuka na kuhamasisha mambo muhimu katika jamii kama ilivyo kwa walimbwende wa tanzania wanavyottumwa kufanya mambo yanayonufaisha jamii.

Diana Kato alifika shuleni hapo kwa lengo la kukutana na wanafaunzi wa shule hiyo na kuwaelismisha juu ya umuhimu wa siku hiyo duniani na kwao pia huko akishirikiana nao katika kufanya jambo hilo.

download latest music    

Diana Kato ambae tangu hapo nyuma amekuwa moja ya mabalozi wanaoshughulikia sana swala la upatikanaji wa maji mashuleni  ilikuwasaidia kujikinga na magonjwa yatokanayo na uchafu.

Hata hivo Diana amesikiliza changamoto mbalimbali zinazopatikana katka shule hiyo na kuahidi kushughulikia anayoweza kwa nafasi yake na kufikisha mengine sehemu zinazohusika.

Wanafunzi wa umoja wakiwa wameshika mabongo ya kuhasisha siku ya kunawa mikono Duniani.

Mikono ya wanafunziwa shue hiyo wakiwa wanafanya zoezi la kunawa mikono na sabuni.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.