Mitandao Ya Kijamii Uganda Yamuumbua Zari

Mama mzazi wa watoto wa Diamond platinumz, Zari the boss ambae pia  anaejulikana kwa utajiri mkubwa Afrika mashariki kutokana na utajiri mkubwa alioachiwa na baba wa watoto wake wa kwanza  Ivan The Don, Zarina Hassan Tlate maarufu kama Zari The Bossy ameumbuliwa na baadhi ya mitandao ya kijamii nchini uganda baada ya kuamua kuweka wazi sehemu asili ambayo alizaliwa mwanamama huyo.

Zari The Bossy ambae amekuwa akipiga picha zenye kuonyesha utajiri wa magari nyumba na vitu vingi vyenye thamani ameripotiwa kuwa ameshindwa kabisa kupaendeleza nyumbani kwao kijijini ambako ndio asili yake.

download latest music    

Zari ambae hivi karibuni alitajwa kama moja ya wanawake matajiri wakubwa nchini Uganda anasemeka kuwa uku Uganda katika kijiji chao kinachojulikana kwa jina la  Jinja hakuna kitu chochote cha maana alichokifanya huku mahali anapoishi yeye na familia yake jijini South Africa ikiwa inaonekana ni ya kitajiri sana.Zari amekuwa akijinadi sana majumba na magari yake yaliyopo Pretoria na Kampala lakini amekuwa akisahau kuwa kuna sehemu aliyozaliwa ambayo pia inatakiwa iendelezwe.

Katika baadhi ya kurasa za mitandao nchi Uganda ziliorodhesha hata mali ambazo mwanamama huyo amekuwa akimiliki na kusema

Zari amekwa akiposti picha akiwa na magari kama Ferrari ,Hummer H2, Lamborgin, na hata Mercedez Benz lakini kitu cha ajabu ni kwamba ukioyeshwa nyumbani kwao huko Jinja lazima utakata kama hapo ndio kwao kwa sababu kwa fedha alizokuwa nazo mwanamama huyo alipaswa kabisa kupatengeneza kwao.Na hata sisi waandishi tunaandika hivyo ili kumkumbusha kuwa ana kwao na mkataaa kwao ni mtumwa wala hatufanyi hivi kwa ubaya wowote ule

Wakielezea historia ya maisha ya mwanamama huyo, mtandao mmoja wa kijamii uliandika kuwa “Mama mzazi wa Zari aliolewa zamani huku Jinja nchi Uganda lakini baadae mama na baba na mama wa Zari walitengena hivyo mama mzazi wa Zari aliamua kuondoka na kuanza kuwalea watoto wake wote nane akiwemo Zari akiwa peke yake, na kuamua kuamia Kampala akiwa na Zari, katika kutafuta Zari alianza kuangaika lakini ikiwa na kutembea na wanaume ili kuweza kujikimu kimaisha ndipo alipokutana na  Ivan The Don na kumjengea mama yake ghorofa iliyopo Munyonyo jijini Kampala.

Ukiachana na utajiri mkubwa alioachiwa na mumewe ambao amezaa nae watoto watutu, Zari pia anajishughulisha na biashara za urembo pamoja na kuanda events za Zari All White Party ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.