Mke wa Roma aeleza alivyozunguka vituo vyote vya polisi kumtafuta mumewe ambaye hajulikani aliko

Image: Roma

Mke wa Roma, Nancy amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mumewe, Roma kupotea. Kulingana na stori mitandaoni kuna fununu kuwa Roma na rafiki yake walichukuliwa na polisi wakiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Kama Watanzania wenzake Nancy hafahamu alipo mumewe ambaye ni baba ya mtoto wake, Ivan. Akizungumza na wanahabari, Nancy ameeleza kuwa amemtafuta mume wake katika vituo vya polisi lakini kila andako hakuna anayerecords za Roma Kutiwa mbaroni. Alisema,

download latest music    

Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu jana saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine. Baada ya hapo nikaanza kutafuta watu wa kunisaidia, baadhi ya ndugu zangu wameangaika vituo vyote vya polisi Roma hayupo, hadi sasa hivi sifahamu yuko wapi, kwa ufupi sina ninachokijua wala ninachokifahamu. Jitihada zangu za kutafuta kwenye vituo vyote vya polisi nimemaliza.

Hivi sasa watanzania kwa ujumla wameungana mikono katika jitihada za kumtafuta Roma ambaye mpaka sasa hajulikani aliko.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua