Mo Music Ndani Ya Bifu Zito na Timbulo

Mwanamuziki wa bongo fleva aliyetamba na vibao kama ‘basi nenda’ No music amefunguka na kudai kuwa anahisi kuwa Timbulo ana bifu naye kwa sababu amekuwa hapokei Simu yake akimtafuta.

Mo music alikuwa chini ya management ya Timbulo na McDenis lakini baada ya muda alihama na kuhamia management nyingine lakini baada ya kuhama aliamua kumaliza bifu na msanii mwenzie Timbulo lakini cha ajabu ameshangaa kuona kuwa anampotezea na kukataa kupokea Simu yake ili waweze maliza tofauti zao.

download latest music    

Mo music ameyaongea hayo kwenye mahojiano na Lilommy ambapo alifunguka mambo yafuatayo;

Kwanza mimi sijawahu kuwa na bifu na Timbulo maana mimi sijawahi kumchunia ila mwenzangu nimejaribu sana kumtafuta nimejaribu sana kumpigia Simu lakini anakuwa hapokei simu yangu lakini mimi namheshimu sana Timbulo maana ni moja ya watu wameweza kunisaidia mimi kuwa Mo music na pia ni kaka yangu alafu isitoshe amewahi kuwa kwenye gemu kuliko mimi kwaiyo kilichotokea ilikuwa ni misunderstanding kati yangu na yeye mimi nilikosea lakini na yeye pia alikosea baadhi ya vitu ambapo kuna mambo aliyazungumza kwenye media badala ya kunitafuta mimi kama mdogo wake tuyamalize wenyewe kwangu mimi niliona kama ameni disrespect kwa kweli”.

Timbulo alipotafutwa ili aongelee ishu hiyo alifunguka na kudai kuwa yeye binafsi hana tatizo na Mo music ila kama kweli hajamkosea ni kwanini ameenda kumuomba radhi redioni?Timbulo amedai kuwa tangu Mo music amehama uongozi amekuwa akitafuta kiki kupitia jina lake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.