Monalisa Adaiwa Kumwaga Machozi Ukumbini

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amedaiwa kuangua kilio ukumbini baada ya kuguswa na mabinti wanatarajia changamoto Kwenye sanaa.

Monalisa alishindwa kujizuia pale alipokuwa anawaongelea jinsi wasichana wadogo wanavyonyanyaswa kingono sehemu wanazokwenda kuomba kusaidiwa ili kuingia katika sanaa.

download latest music    

Monalisa aliangua kilio hicho ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo alikuwa akizindua mpango wa kuwaendeleza mabinti wenye vipaji vya kuigiza uitwao Monalisa ACT.

Mona alifunguka kuwa anajua mabinti wengi wakienda kwa watu kuomba kusaidiwa ili waoneshe vipaji vyao, wengi huishia kudhalilishwa kingono ndipo wasaidiwe, jambo ambalo alililaani vikali.

Ukweli mabinti wengi wana vipaji vya filamu lakini wanaishia kukata tamaa na vipaji vyao kupotea, hii ni kwa sababu wanapokwenda kuomba msaada wameishia kuombwa rushwa ya ngono, jambo ambalo siyo zuri kabisa“.

Alifunguka Mona huku machozi yakimlengalenga na hata aliposhuka na kwenda kuwakumbatia baadhi ya mabinti alijikuta akilia.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.