Monalisa Akabidhiwa Bendera Kupeperusha Nchi Ghana

Mwanadada Monalisa ambae ni msanii mkongwe sana katika tasnia ya filamu amekabidhiwa bendera ya taifa pamoja na ticket ya ndege na Mh  waziri wa michezo Harrison Mwakyembe kwa ajili ya safari yake ya kwenda Ghana ambapo ataenda kuepeperusha bendera ya Taifa katika maswala ya tasnia ya filamu kutokana na kuchaguliwa kwake katika kuwania tuzo za African Prestigious Award nchini humo .

Monalisa ambae alisindikizwa na mama yake  katika makabidhiano hayo katika ofisi za Baraza  walihudhuria pia watu mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Habari sanaa na Michezo Mh .Juliana Shonza pamoja na katibu mtendaji wa baraza la sanaa tanzania.

download latest music    

Monalisa anakwenda kuiwakilisha Tanzania baada ya kuchaguliwa katika kategoria hiyo na kuomba watanzania na afrika kwa ujumla kumpiagia kura kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja sasa.Kila la kheri kwake.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.