Monalisa Akiri Kumkumbuka Tyson Baada Ya Matokeo Ya Mtoto Wake

Msanii mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kukiri Kumkumbuka baba wa mtoto wake Marehemu George Otieno ‘Tyson’ katika kipindi hiki.

Monalisa amekiri kuwa baada ya mwanaye Sonia George Tyson kufaulu kidato cha nne na kupata daraja la kwanza huku somo la Hesabu akiwa amepata A, ame­jikuta akibubujikwa machozi ya fu­raha na kutamani uwepo wa baba wa Sonia, George Tyson aliyetan­gulia mbele ya haki.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wik­ienda, Monalisa alisema kuwa alipopata taarifa hizo alishindwa hata kulala lakini kingine kilichowa­tia huzuni ndani ya furaha hiyo ni baa­da ya kukumbuka kwamba baba yake huyo alikuwa akipenda sana mtoto wake huyo asome sana ili aweze kufika elimu ya juu.

Siwezi kusema furaha ambayo ninayo kwa mtoto wangu huyo lakini Tyson angekuwepo ange­shuhudia ukuu wa Mungu, kwa sababu alipenda sana Sonia asome tena aongoze kitaifa, ndio kitu alichokuwa akikipenda lakini tunashukuru Mungu kwa kuibuka na daraja la kwanza kwani ni wengi waliotamani lakini wameshindwa kupata, yeye amewe­za”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.