Monalisa Awatolea Povu Wanaomuita ‘Bibi’

Muigizaji mkongwe wa filamu za Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Mobalisa amewatolea Povu zito watu ambao walimuita bibi Baada ya kuonekana kwenye video ya msanii Ben Pol.

Mwezi uliopita Staa wa Bongo fleva Ben Pol aliachia video yake ya wimbo wake wa Ntala Nawe na ndani yake alimuweka Monalisa Kama Video Queen Wake uwamuzi uliozua hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Monalisa amefunguka na kusema hakushangaa comments za mashabiki wa Ben Pol waliomuhoji kwanini hakuchukua Wasichana wadogo wa kuendana naye.

Kila mtu ana mtazamo Wake na kwangu Mimi hicho ni kitu cha kawaida  watu lazima tu wataongea midomo wameumbiwa ili kuongea ila poleni sana na itabidi tu muangalie video kwa sababu Ben Pol ndiye mtu ambaye amenichagua na ameona ninapendeza kwenye video yake”.

Lakini pia Monalisa ameweka wazi kuwa yeye ni shabiki namba moja muziki wa Ben Pol hivyo alipopata nafasi ya kuwa video queen alikuwa tayari hata kufanya bila malipo lakini Ben alimpa kiasi fulani cha pesa ambapo halukitaja hadharani.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.