Monalisa na Mwanaye Washangaza Umati Kwa Hili

Msanii mkongwe wa Bongo movie Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa na Mtoto Wake Sonia walishangaza watu Baada ya kuonekana wakiangua kilio mbele ya hadhara.

Monalisa na Mwanaye walishikwa na huzuni na kuanza kulia walipokuwa wakikabidhi misaada kwenye kituo cha kulea watoto yatima cha Yoko kilichopo Mbezi- Mwisho jijini Dar.

download latest music    

Aliyeanza kulia ni mtoto wa staa huyo, Sonia baada ya kupewa kipaza sauti azungumze ambapo alishindwa, akaanza kulia huku mama yake akimkumbatia, wakajikuta wakilia pamoja na baadae Watoto wa kituo kile nao walionekana wakilia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, rafiki wa karibu wa Sonia ambaye alikuwa ameongozana nao alitoa sababu iliyomfanya mpaka akaanza kulia:

Masikini Sonia, anaonekana ana huru­ma na machozi yanamtoka kwa sababu na yeye anakumbuka amempoteza baba yake pia”.

Monalisa alifunguka na kusema kuwa ameamua kujitoa kusaidia wazo hilo la mtoto wake kwa sababu ameona anafanya jambo jema.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.