Monalisa na Ray Kigosi Wang’aa Kwa Tuzo Nchini Ghana

Muigizaji wa Bongo movie Yvonne Cherry kwa Jina maarufu la usanii kama Monalisa ameng’aa kwenye tuzo za African Prestigious Awards (APA) zilizofanyika nchini Ghana.

Monalisa ameshinda tuzo kwenye kipengele cha Muigizaji bora wa kike nchini Africa. Tuzo hizo zilitolewa Siku mbili zilizopita.

download latest music    

Lakini pia Ray Vicent Kigosi pia ameibuka kidedea baada ya kukwapua tuzo ya Muigizaji bora wa kiume barani Africa huku wasanii kama Mzee majuto alibahatika kuchaguliwa kushindania Tuzo hizo.

Lakini pia Monalisa alipokea tuzo kwa niaba ya Raisi John Pombe Magufuli ambaye ameshinda tuzo kwenye kipengele cha Uongozi bora.

Kwa upande mwingine, Mtanzania Moise Hussein ameshinda tuzo hizo kwenye kipengele cha mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.