Monalisah Ashinda Tuzo Nyingine Nchini Marekani

Muigizaji Mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisah ameibuka kidedea baada ya kupokea tuzo kutoka katika tuzo za The African Film Festival (TAFF) zilizofanyika nchini Marekani.

Miezi michache iliyopita Monalisah alipokea tuzo nyingine kutoka katika tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. Tuzo hizo zilitolewa Accra nchini Ghana.

download latest music    

Mona amedai safari hii hakujua kama anaenda kupewa tuzo kwani alienda Kwenye hafla hiyo kama host.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Monalisah amefubguka haya:

Namshukuru Mungu sana kwa anayonitendea, sikujua lolote kuhusu Tuzo, nilialikwa kama Host wa usiku wa Tuzo na kushiriki Tamasha la Filamu. Kumbe TAFF walikuwa wana nia ya kunizawadia Tuzo hii Wow!.

Sijui niseme nini mtoto wa Natasha Mimi?watu wa nje wananielewa kiasi hiki kwa kitu ninachofanya kwa ajili ya nchi yangu?ni hisia ambazo siwezi kuelezea“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.