Moni aeleza kilichotokea alipotekwa nyara aliwa na Roma Mkatoliki

Moni Centrozone amefunguka kuhusu tukio lililofanyika karibu mwezi moja uliopita – alitekwa nyara na watu wasiojulikana akiwa studio.

Rapper huyo alitekwa nyara akiwa na Roma Mkatoliki, producer Bin Laden na Imma wakiwa katika studio za Tongwe Records.

download latest music    
Roma Mkatoliki na Moni Centrozone

Moni alisimulia kilichofanya katika kipindi cha XXL cha Clouds FM. Soma maneno aliyosema hapo chini:

“Yule jamaa wakati ananiambia nimpe simu ya Roma, wakati naifata simu ya Roma akawa ameshaingia akaiwahi, akaichukua akaniambia wewe ndo Moni? Wewe ndio sembe sembe dona? Kaa hapo chini nimekwambia, kaa kwenye kochi simu yako iko wapi? Nikamwambia simu yangu ipo kwenye chaji, akamuuliza na Bin Laden, naye Bin Laden akatoa simu. Akauliza Junior yuko wapi? Mpigie J-Murder sasa ile hali ya vitisho ikawa imeshaanza,

“Kumpigia J-Murder hata kabla sijamaliza maelezo yaani ile bosi kuna watu wamekuja hapa studio, jamaa akanipora simu. Oya inakuwaje J-Murder, sisi hapa tunataka kurecord, tunataka kurecord nyimbo sita.

“Muda ambao nakumbuka nimesali sala zangu za mwisho ni ule pale, nikaona dah basi kama kuna kitu nimefanya au kuna kitu nimekosea basi ni kumuachia Mungu,” Moni Centrozone alisimulia kilichotokea.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere