Moni Centrozone Afungukia Bifu Lake na Roma

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Moni Centrozone amefunguka na kuongelea bifu lake na msanii mwenzake Roma.

Roma alikuwa ni mmoja kati ya watu wa karibu wa Moni kwa muda mrefu walikuwa washkaji na walikuwa wanaonekana wote pamoja lakini Miezi ya hivi karibuni ukaribu huo umepotea.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Millard Ayo, Moni anafunguka na kuweka wazi kuwa sababu kubwa iliyofanya wawili hao kupoteza ukaribu ni baada ya Roma kuingia kwenye group na Stamina (Rostam) bila kumpa taarifa yoyote.

Mimi na Roma hatuna ushkaji tangu alipoamua kufanya projects zake na Stamina bila kunipa mimi taarifa kwaiyo nikaona kama nimepunguzwa bila kufanya kosa lolote ndipo na nilipoamua kujiongeza na kuamua kufanya kazi mwenyewe.

Tangu hapo nimefanya projects kadhaa kama matango pori, Bongo supastaa na kusema ukweli nimeweza kufanya vizuri mwenyewe na maisha yanasonga”.

Moni amesisitiza kuwa hana bifu na Roma kwa sasa Lakini pia hana urafiki naye na hataweza kufanya nae kolabo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.