Moni na Nai Waamua Kurudiana Rasmi

Msanii wa Bongo fleva nchini anayefanya miondoko ya Hip Hop Moni Centrozone amerudisha majeshi yake kwa mpenzi wake video vixen Nai.

Wiki kadhaa zilizopita Moni na Nai walisikika sana Kwenye Media mbali mbali wakirushiana maneno baada ya kuachana ambapo kulikuwa na tuhuma nyingi kama vile michepuko.

download latest music    

Nai alimtuhumu Moni kwa kumpiga na hata kudai ana michepuko mingi akiwemo mmoja wa marafiki wa Gigy Money.

Kwenye Interview na Wasafi Tv Moni na Nai wamethibitisha kurudiana na kuweka wazi kuwa wameamua kuweka tofauti zao pembeni:

Kwa sasa tupo sawa lakini haya ni mambo ya ndani japo kuna kukosana na kuelewana lakini siri zetu za ndani ambazo tunajua wenyewe tunamalizana vipi”.

Wapenzi hao waliweka wazi kuwa ni jambo la kawaida katika mapenzi kugombana na kwa kuwa wanapendana hivyo wameamua kurudiana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.