Mose Iyobo Afungukia Mipango Ya Ndoa Na Aunty Ezekiel

Dansa maarufu wa staa Diamond Platnumz, Mose Iyobo ambaye pia ni Mpenzi na mzazi mwenzake ambaye pia ni staa wa Bongo movie nchini Aunty Ezekiel.

Iyobo amesema kuwa hana muda wa kukaa na kusikiliza watu wanasema nini kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mapenzi yake na Aunty kwani anampenda na lazima atamuoa tu.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Iyobo alisema wapo watu wanaotamani siku moja waachane lakini anajua ni kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa kuwa mizizi ya penzi lao imekwenda chini sana.

Mimi natarajia kumuoa Aunt kwani ana kila sifa ya kuwa mke wangu, na nitakuwa mfano bora kwa mastaa wote na kuondoa ile dhana kuwa mastaa hawadumu kwenye ndoa”.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi kuwa penzi la wawili hao limeingia doa Baada ya kutoonekana pamoja kwa muda mrefu na kusemekana kuwa wameachana.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.