Mose Iyobo Akanusha Kuwa na Mgogoro na Mama Cookie

Dancer maarfu wa msanii mkubwa nchini Diamond Platinumz kutokea wasafi anaejulikana kama Moze Iyobo aMefungukia ishu inayoendelea mitandaoni kuwa yeye na mzazi mwenzie mama cookie maarufu kama Aunty Ezekiel kuwa wapo katika mgogoro wa kutaka kuachana kuwa sio kweli hata kidogo.Mose Iyobo amesema kuwa watu wamekuwa wakitasfiri vibaya baadhi ya meseji na vitu wanavyoviona katika mitandao ya kijamii bila kujua kwanini mtu ameamua kuweka post flani katika ukurasa wake.

Hivi karibuni Aunty Ezekiel aliwka post ilikuwa ikiashiria kuwa ana matatizo katika mahusiano yake,ambapo hii iliibua hisia tofauti kwa mashabiki wake na kusema kuwa inawezekana msanii huyo kwa sasa amambo yake yameenda kombo kati yake na mpenzi wake.

download latest music    

Hata hivyo hayo yote yalikuja kujiweka wazi pale  moze alipoamua kuweka maoni yake katika moja ya videoa alizochapisha mama cookie tena katika ukirasa wake wa instagram ambapo moze iyobo aliandiaka “umeninyima mapenzi alafu  upost, freshi?” kitu kilichowafanya mashabiki kupigia mstari na kupata jawabu kuwa wawili hao wako katika mgogoro.

Akiongea na gazeti la Ijumaa Mose Iyobo aliamua kuliongelea hilo na kusema kuwa wao wameishi kwa muda mrefu na kwa sasa wamekuwa watani sana kiasi kwamba wanaweza kutaniana hata katika mitandoa ya kijamii,

unajua watu wanashndwa kuelewa kuwa  mimi na mama cookie tunataniana sana,kwiao hata mimi kuandika vile katika instagram  ilikuwa ni kumtania tu lakini watu wamekuja wametokwa na mapovu.-Alisema Mose Iyobo.

Mahusiano kati ya mose na aunty yameanza miaka kama minne aliyopita na ni moja ya couple ambayo imekuwa na heshima bila kuwa na skendo za hapa na pale tangu ianze, ingawa wasanii wa watu wengi maarufu wamekuwa wakiingia katika mahusiano na kuachana kwa muda mfupi hii imekuwa ni tofauti na kwao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.