Mose Iyobo na Tunda Warushiana Maneno Kisa Pombe

Dancer maarufu kutoka keen he label ya WCB, Mose Iyobo ameingia kwenye vita ya maneno na matusi na mrembo Tunda baada ya kutuhumiwa kuzulumu shilingi laki moja ya pombe ya Belaire.

Siku ya jana Aunty Ezekiel alianzisha kizaazaa na Tunda baada ya kuingia kwenye ukurasa wake wa Instagram na  kumdai pesa taslimu shilingi laki moja ambayo alimkopeshea pombe anzouza aina ya Beleire.

download latest music    

Lakini baada ya kudaiwa pesa hizo mara kadhaa Tunda alidai kuwa alipoenda kuilipia chupa hiyo Dukani kwao Aunty Ezekiel hakuwepo hivyo mtu aliyekuwepo alikuwa ni Iyobo ambaye ndiye aliyemkabidhi pesa hizo lakini alishangaa alipokutana na Aunty juzi akamdai wakati alishampa mumewe Iyobo.

Baada ya kuambiwa maneno hayo Iyobo aling’aka vibaya mno na kukana tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hakupewa pesa hizo ndipo alipomtolea povu zito Tunda ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika maneno haya:

Ujinga nikubishana na mtu ambaye ameshafanya mambo yote ambayo wewe unafanya leo kama marudio unachotakiwa useme ni sina hiyo hela ntalipa siku fulani na sio kuanza kuongea ushamba  hawezi kutafuta kiki kwako ana mtoto maarufu kushinda wewe alafu kingine benten ni baba yako aliyekuzaa akashindwa kukupeleka shule umeishia kufumuliwa free unakosa laki ya kununulia pombe”.

Baada ya kutolewa povu hilo na Iyobo na Tunda naye alifunguka yaliyo moyoni mwake na kumjibu ambapo alimwandikia ujumbe huu :

Alafu na wewe Mose unakaa chini unaandika upuuzi kama huo kama ni kweli ni wewe umeandika basi huna Uso wa haya! Sasa nakuuliza swali moja tu kwa nini ulinoblock kukupigia kipindi Aunty ameanza kuniuliza kuhsu hela? Sikilizeni nyie hebu nitoleeni upuuzi wenu watu wazima mliokosa busara na akili kabisa yaani mimi nigombane na nyie Kisa laki moja? Kiukweli hata kama ningekuwa sina pesa siwezi kukosa laki “.

Lakini unakumbuka pale ambapo Mose aliposema mwanangu Cookie maarufu kuliko we we? Basi Funds alifika mbali katika ugomvi huo na kumuingiza mtoto wao kwa kumuita mtoto mbaya Tanzania nzima.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.