Mr. Nice akana kuibiwa katika sherehe ya kuapishwa kwa gavana wa Nairobi (Picha)

Mr. Nice alikua miongoni mwa wasanii na watu mashuhuri ambao walihuduria hafla ya kuapishwa kwa gavana mpya wa jimbo la Nairobi – Mike Mbuvi Sonko.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na makamo wake William Ruto pia walihudhuria sherehe hio ambayo iliandaliwa jana Agosti 21 jijini Nairobi.

download latest music    
Mr. Nice na Bahati wakiwa kwa hafla ya kuapishwa kwa gavana Sonko

Awali kulikuwa na repoti kwenye mtandao kuwa Mr. Nice aliibiwa baadhi ya vitu alipokuwa akitangamana na mashabiki katika hafla hio. Hata hivyo Mr. Nice amekana madai kuwa aliibiwa.

“Waandishi vilaza mnapenda kurukia sana hata msilolijua mimi katika show ya kuapishwa Sonko leo sijaibiwa na mtu yoyote. Kifupi ni kwamba mashabiki waling’ang’ana kucheza na mimi na bahati mbaya wakajikuta wamekata cheni zangu na pia leseni yangu ikadondoka nilikuwa nayo kwa mfuko wa koti la suti,” Mr. Nice aliandika kwa Facebook.

  

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere