Mr Nice Atupa Jiwe Gizani,Yasemekana Alimlenga H.Baba

Moja ya wasanii wakongwe nchini aliyevuma sana hapo awali kwa style yake ya kucheza ikijulikana kama takeu ambayo ilipendwa sana na watoto Lucas Mkenda maarufu kama Mr.Nice amerusha jiwe gizani na kumponda moja ya wasanii wenzake wakongwe ambae pia kwa sasa yupo kimya.

Akiongea na East Africa alipokuwa akitambulisha wimbo wake mpya hivi karibuni , Mr. Nice anasema kuwa kuna baadhi ya wasanii katika game walikuwa wakisafiria nyota yake katika muziki huku wakiiga anavyoimba hadi kucheza lakini cha ajabu ni kwamba sasa hivi wamefulia na wameshindwa kuinuka tena.

download latest music    

Watu walikuja kwenye game, wakataka kutumia style yangu ya takeu na kuitumia kabisa  na bado wakashindwa, wakaingia bongo movies na huko nako pia kukawashinda.

Hata hivyo maneno hayo yanasemekana kutupiwa msanii mwenzie mkongwe h.baba kutokana na wasifu huo kumfanania kabisa msanii huo kwa sababu kwa kipindi cha style ya takeu ambapo Mr.Nice ndie aliekuwa mwanzilishi lakini h.baba nae alikuja na kuimba huku akicheza style hiyo hiyo.

H.Baba pia aliingia katika tasnia ya filamu na kufanya vizuri pia ingawa kwa sasa haijulikana msanii huyo yuko wapi kutokana na ukimya wake kwa muda mrefu.

Hata hivyo Mr.Nice alipoulizwa kuhusu kwanini amekuwa akitumia muda mrefu kuweka makazi yake nchini kenya , msanii huyo alisema kuwa amegundua kuwa kenya amekuwa na mashabiki wengi sana na kazi zake zinapendwa sana nchini kenya kulikio huko,Mr.Nice ametambulisha wimbo wake mpya baada ya kukaa kimya katika game kwa muda mrefu sana.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.