Mr. Nice Hakuna Msanii Mkali Zaidi Yangu Duniani

Msanii mkali na mkongwe aliyetamba miaka ya nyuma kwa nyimbo zake kama kikulacho, rafiki yangu na Fagilia na nyinginezo nyingi zilizosindikizwa kwa staili yake ya kipekee ya Takeu Style.

Tangu miaka hiyo mpaka leo hii kuna mambo mengi yaliyotokea lakini hasa lililochukua nafasi kubwa ni tetesi zilizokuwa zinaenea. Moja kati ya tetesi zilizoenea kwa kasi ni ugonjwa aliokuwa nao Mr. Nice ambapo wengi walizusha kuwa anaumwa ukimwi na amefulia hana mbele wala nyuma.

download latest music    

Siku za hivi karibuni Mr. Nice amerudi tena ghafla kwenye vyombo vya habari ambapo ni juzi tu alisikika kurudi kwenye bifu tena na aliyekuwa hasimu wake Mkubwa miaka ya nyuma msanii nwenzake Dudubaya lakini pia alitawala vichwa vya habari baada yaya kuingia kwenye sintofahamu na Young Dee.

Kwenye mahojiano na LilOmmy Mr. Nice amefunguka hayo yote na kusisitiza kuwa anaamini hakuna msanii mkubwa duniani kama yeye mwenyewe:

Kwangu mimi hakuna msanii yoyote ninaye mkubali zaidi yangu mimi mwenyewe yaani Mr. Nice ndiye Msanii ninayemkubali na kumheshimu sana  na ninapenda kusema kwa nini najiheshimu mwenyewe, ni kwa sababu naamini ni lazima ujipende wewe kabla haujampenda mwenzio kwaiyo kwa wasanii wenzangu wote sioni wa zaidi yangu kwaiyo nimimikwanza halafu wao ndio wanafata”.

Lakini Mr. Nice amefunguka na kudai kuwa tetesi za yeye kufulia sio za kweli kabisa kwani anaishi maisha mazuri na pia anasaidia watu wengi wasiojiweza lakini pia anamuangalia Mama yake mzazi ambapo anaamini mama take anaishi maisha mazuri kuliko mama wengi duniani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.