Mrembo Aliechora Tatoo Ya Msami Afunguka

Mwanadada ambae alipata umaarufu mkubwa siku za nyuma kutokana na kuwa na mahusiano na msanii wa kisingeli Dullah makabila, na baadae kuingia katika ugomvi na Husna Sajenti baada ya kuachana msanii huyo huku chanzo kikisemekana kuwa ni mwandada Husna. Ameamua kufunguka kuhusu mahusiano yake na msanii Msami Baby na kuhusu swala la yeye kuchora tatoo yenye jina la msanii huyo.

Wiki iliyopita msanii wa muziki anayefanya vizuri katika kuimba na kucheza pia Msami, aliongea kuwa yeye hana mahusiano na msichana yeyote kwa sasa na kama atakuwa na mahusiano angeyaweka wazi lakini amekuwa akimjua msichana huyo anaeitwa Asali na amesikia kuwa amechora tatoo ya jina lake lakini hana mahusiano nae yoyote isipokuwa wanafahamiana kwa kwasababu anakaa karibu na  nyumba ya mama yake.

download latest music    

Akiongea na eNews ya EATV, mwanadada Asali amekiri kweli kuwa amechora tatoo lakini kama shabiki tu na rafiki wa karibu wa msanii huyo kwa sababu wanakaa mtaa mmoja  na amekuwa akipita kwao mara kwa mara, lakini pia ni rafiki yake anaempenda na kumkubali  kama shabiki”Ni rafiki yangu, nampenda namkubali,napenda muziki wake,napenda hata anavyokatika lakini kitu cha kushangaza nimeona juzi anaongelea mambo yale, hakupaswa kuongelea mambo yale kabisa kwa sababu hata mimi siwezi kuwa nae na sijawaza kuwa nae” aliongea Asali

Asali ambae mara ya kwanza alikuwa na mahusiano na msanii Dullah Makabila alipoulizwa kati ya Dullah Makabila na Msami ni mwanaume gani anaenjoy akiwa nae aliitika na kusema kuwa akiwa na Msami ana-enjoy zaidi ilihali mara ya kwanza alikataa kuwa hana mahusiano yoyote na Msami wala hana hisia nae.

Asali alisema kuwa kwa sasa hana mahusiano na mtu yoyote lakini kitendo cha Msami kumwambia kuwa hawezi kuwa nae kwenye mahusino kimemkera kwa sababu hajui maneno hayo yamtokea wapi ilihali hata yeye pia hakuwahi kuwaza kuwa na mahusinao nae zaidi ya kuwa marafiki  na kuwa anamkubali kama shabiki wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.