Mrembo Wa Miaka 19 Amtongoza Millard Ayo

Mwanadada mmoja wa miaka 19 inaesemekana kuwa ni mtangazji wa kituo kimoja cha radio jijini Dar, amejitokeza na kuamua kufunguka kuelezea hisia zake kwa mtangazji mkongwe na maarufu nje na ndani ya Tanzania Milard Ayo katika ukurasa wake wa Instagram,

Mwanadada huyo aliejulikana kwa jina la Susan Labia amekiri kuumiza kwa muda mrefu na hisia za kimapenzi kwa milaard ayo hivyo ameshindwa kuvumilia kwa sababu anaona anazidi kuumia sana wakati ana uwezo wa kufikisha meseji hiyo kwa mwanaume anaempenda.

download latest music    

Susy anasema kuwa  uamuzi wake unaweza kumkwaza milaard ayo kwa sababu hajui kama yuko katika mahusiano lakini aliona ni bora aongee ukweli wake ili ata kama atakufa basi asife na kitu moyoni mwake. na anajua kuwa inawezekana hata millard ayo asiione meseji yake lakini atambue kuwa kuna mwanamke anampenda sana hata kama hatopata bahati ya kuwa nae.

Susan anaendelea kusema kuwa pamoja na kwamba hakusoma kufika mbali kwa sababu hakusomeshwa lakini ana akili kubwa ya maisha kwaoi anamuomba Millard asimdharau kwa hilo  kwa sababu anamuona milaard ni mtu mwenye huruma na ni mstaarabu anafaa sana kuwa   mume wake.

Mrembo Susan na kile alichokiandika katika ukurasa wake wa instagram kuhusu hisia zake kwa Milaard ayo.

Inaweza kuwa ni kitu cha kustaajabisha kidogo kwa mwanamke kufunguka na kueleza hisia zake kwa mwanume kwa sababu imeshazoeleka kuwa mwanaume ndio anakuwa na fursa ya kumfata mwanamke lakini hii imekuwa tofauti kwa Susan ambae aliona akinyamaza kimya mwanaume anaempenda hatopata na kujua kile anachojisia yeye.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.