Mrisho Mpoto Amtaka Steve Nyerere Apunguze Gubu Baada Ya Kukosa Tuzo

Msanii maarufu Bongo Mrisho Mpoto amemuoa juu msanii mwenzake wa Bongo movie Steve Nyerere kumtaka apunguze gubu na kukubali matokeo baada ya kukosa tuzo za SZIFF.

Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival zilifanyika wikiendi iliyopita na kuleta gumzo baada ya wasanii waliokosa tuzo kama Steve Nyerere kuanza kulalamika.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya siku chache zilizopita na Bongo 5 Steve Nyerere alilalamika yeye kukosa tuzo Lakini pia alidai pia kuna wasanii ambao angependa wapate tuzo lakini walikuwa kama vile Aunty Ezekiel, JB na wengineo.

Mrisho Mpoto amempa makavu na kumwambia aache kulalamika kwa sababu ameshindwa hilo ni gubu badala yake afanye juhudi ili Safari ijayo aweze kupata tuzo hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mrisho Mpoto ameandika mambo haya:

Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo.

Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…

Zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.