Mrisho Mpoto- Wasanii Kuoa Nje Ya Nchi Kuna Tatizo na Wanahitaji Kufundwa

Mwanamuziki wa Muziki wa Asili  Mrisho Mpoto amefunguka kuhusu trend mpya ya mastaa mbali mbali wa Bongo fleva kuamua kwenda kuoa nje ya nchi.

Mrisho Mpoto amefunguka na kudai nyimbo yake inayofanya vizuri ya ‘Nimwage Radhi’ aliyomshirikisha Harmonize imetoka a na wasanii wanaoa nje ya nchi.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Times Fm,  Mpoto alitoa kauli hiyo  pale alipoeleza kuwa awali alishauriwa na Harmonize video hiyo ikafanyike Nigeria au Afrika Kusini ila akakataa kutokana ujumbe wa wimbo huo ni kwa ajili ya Watanzania.

Kwa sababu wimbo mimi naongea na Watanzania, nilikuwa nimeguswa na jinsi vijana wetu wa Kitanzania wanavyokwenda kuoa nje ya Tanzania, kwa nini vijana wetu maarufu hawataki kuoa nyumbani?.

Nikaliona hilo, nikajua kuna tatizo hapa, hawa wanahitaji kufundwa, hawa kuna maneno wanatakiwa kuambiwa, waambie na mwenye maneno yake”.

Siku za hivi karibuni tumeshuhudia mastaa mbali mbali wakienda kuoa nje ya nchi kama vile Ali kiba aliyemuoa binti Amina kutoka Kenya, AY alimuoa Mwanamke kutoka Rwanda na hata Stamina alimuoa binti kutoka Rwanda.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.