Msanii Aliyejitolea Kumuoa Zari Ajitamba Kuwa Ana Pesa Kuliko Diamond

Msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya anayejulikana kama Alex Apoko ‘Ringtone’ ameibuka tena na kudai ana pesa nyingi kuliko msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Ringtone amezidi kumtaja Zari akubali kuolewa naye kwani amemhakikishia kwa pesa nyingi alizokuwa nazo atamtunza vizuri sana kuliko hata Diamond ambavyo angeweza.

download latest music    

Ringtone alifunguka hivi karibuni kwenye mahojiano aliyofanya na Citizen Tv ambapo alijitapa kuwa kama mjasiriamali alitengeza milioni moja yake akiwa mwanafunzi alipoanza kuuza cd zake za muziki lakini pia amejitapa kuwa ana biashara zake kwenye sekta ya afya na nyinginezo.

Msanii huyo amejitapa ana pesa za kutosha za kuweza kumlea Zari pamoja na watoto wake wote na pia Zari ni mwanamke mzuri na wa gharama ndio maana Diamond ameshindwa kumuhudumia alijaribu kwa miaka mitatu lakini ameshindwa kuendelea lakini yeye yupo tayari.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtone alimuwekea Zari ujumbe huu:

Dear Zari Jesus loves you so much na amenitumia mimi leo kukwambia ana mipango poa na wewe. Mimi alinitoa from the streets mahala sikuwa na family, nyumba hata lishe buy now na magari, hela na magari ninavyo tele. Don’t waste time you never know tomorrow. I love you tha same way God loves you”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.