Msanii Coyo Apewa Kichapo na Mashabiki Kwenye Shoo Tarime

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha Nyakanyaka, Coyo amedaiwa kutembezewa kipigo kizito na mashabiki zake kwenye shoo aliyofanya Tarime.

Shilawadu wanaripoti kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita Coyo alikuwa anafanya shoo mbili moja Ikiwa ni Kenya na nyingine upande wa Tanzania kwa kuwa pale ni mpakani.

download latest music    

Lakini inasemekana alivyomaliza shoo ya Kenya alikuwa ana mpango wa kuwahi Tarime na kwenda kumaliza shoo ya Tanzania lakini usiku mnene ulikuwa umeshaingia hivyo alichelewa kufika na kukuta mashabiki wamevimba.

Unaambiwa alivyofika mashabiki hawakutaka maneno walianza kumtukana matusi mazito na ile anatoka nje wakamdaka wakampa kipigo kitakatifu mpaka Promota alipoenda kumuokoa.

Kwenye mahojiano na Soudy Brown, Coyo alikataa taarifa hizo na kudai kuwa hakuenda Kenya kufanya shoo bali alienda kusalimia marafiki lakini aliporudi kufanya shoo alitaka kufanyiwa utapeli na promota wa shoo yake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.