Msanii mpya wa Wasafi Records Lava Lava azindua video ya wimbo wake-Bora Tuachane

Image: Lava Lava

Lava Lava ameachia wimbo mpya Bora Tuachane ambao unawazingua wengi Afrika Mashariki. Tangu Diamond Platnumz kumtambulisha kama msanii wa Wasafi…Lava Lava amepata mashabiki wengi kwa muda mfupi kuonyesha kuwa yuko tayari kuwatumbuiza wengi.

Hata hivyo Lava Lava ameachia video yake ya kwanza tangu kuingia Wasafi. Video hii imekuja siku mbili tangu kuachia audio.

download latest music    

Mashabiki nao pia wameonekana kumpa support msanii huyu ambaye kwa hivi sasa anawazingua wengi. Sauti yake pia ni ya kumtoa nyoka pangoni na inaonekana kuwa atawapa Harmonize, Rayvanny na Rich Mavoko competition ya kutosha. Tazama video hiyo hapa.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua