Msanii Ringtone Azidi Kumlilia Zari Atangaza Kumnunulia Range Rover

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya Ringtone Apoko amezidi kulilia penzi la Zari The Bosslady ambapo siku ya jana ametangaza kumnunulia gari aina ya Range Rover.

Siku za nyuma Ringtone alishawahi kutangaza penzi lake kwa Zari na hata kuhahidi kumuoa huku akidai anahitaji mwanaume ambaye ni mcha Mungu na aachane na Diamond.

download latest music    

Siku ya jana Zari alitua nchini Kenya tayari kwa ajili ya kuhudhuria Tamasha la hisani linaloitwa Colour Purple Concert lililoandaliwa na litakalofanyika tarehe 12.

Baada ya Ringtone kupata taarifa kuwa Zari anatua nchini Kenya mara moja alimjulisha akifika atakuta gari lake Range Rover limeshanunuliwa na linamsubiri.

Siku chache zilizopita Zari alijinunulia Range Rover Sport lenye thamani ya shilingi milioni 175 lakini pia aliweka wazi kuwa kuna msururu mrefu wa wanaume wanaotaka kuwa naye.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.