Mshindi wa BSS Kuzawadia Milion 50

Kiongozi wa mashindano ya muziki ya BSS Tanzania Madam Ritha ametangaza kuwa zawadi kubwa atakayopewa mshindi ni shilingi milioni 50 za kitanzania ingawa pesa hizo hatopewa zote kwa mara moja.

Madam Ritha anasema kuwa wameamua kutoa pesa hizo kwa  awamu kwa sababu  kumekuwa na washindi ambao hawanufaiki na pesa hizo hasa wanapokabidhiwa zote kwa mara moja.

download latest music    

Akifafanua kwa undani zaidi, Madam Ritha anasema kuwa Mshindi atakuwa akipewa pesa hizo kila mwezi shilingi mil 1.2 lakini milion 5 za mwanzo atakabidhiwa kwa mara moja siku ya tukio.

Hata hivyo pia msanii huyo aatanza kufanya kazi chini ya Switch Rekodi ambao wameweza kuwakabidhi kwao na tayari walishasaini mkataba tayari.

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.