Mtoto wa Ray Apata Dili Nono Kutoka NMB

Mtoto wa wasanii Ray Kigosi na Chuchu Hans  anaejulikana kwa jina la Jarden amepata dili nono la kuwa balozi wa  benki ya NMB baada ya baba yake kuamua kumfungulia akaunti katika benki hiyo na benki hiyo kuamua kumchukua kama balozi kwa watoto wengine ambao wazazi wao watataka kuwafungulia akaunti katika benki hiyo kwa ajili ya matumizi ya watoto wao hapo baaadae hasa katika masomo yao.

Akizungumza na waadnishi wa habari alipokuwa katika makao makuu ya benki hiyo jijin Dar, Ray Kigosi ambae ndie baba wa mtoto amesema kuwa aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kushauriana na mama wa mtoto (Chuchu Hans) baada ya kuona kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa huduma nzuri kwa wateja wao na pia kwa sababu ya huduma hiyo mpya ya akaunti za watoto.

download latest music    

niwaombe tu wasaii wenzangu kuwa ni vizuri kumfungulia mtoto akaunti benki,hili ni swala muhimu sana kwa sababu sisi wazazi leo tupo laini hatujui kesho yetu itakuwaje.-Alisema Ray Kigosi akitoa ushauri kwa wasanii wenzake .

Pia ili usimnyime mwanao haki ya maisha mazuri mtoto wako  hapo baadae basi ni vizuri kuchukua uamuzi wa kumfungulia mtoto  ili kama wewe usipoweza kwa wakati huo unajua ataweza kusoma kwa akiba uliyomuekea.

Katika ufunguzi wa akaunti hiyo Ray alikuwa pamoja na mzazi mwenzie Chuchu Hans pamoja na mtoto wao Jarden.

Kwa kuongezea umahasishaji , meneja wa benki hiyo anatoa wito kwa wazazi wote kuwafungulia watoto wao akaunti ili kuwasaidia katika maisha ya baadae.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.