Mtoto Wangu wa Tatu Nitazaa na Mwanaume Atakayenioa-Hamisa Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa endapo atazaa mtoto mwingine basi atazaa na mwanaume atakuwa amemuoa.

Hamisa ambaye tayari ana watoto wawili ambao kila mmoja ana Baba yake ambaye mmoja amezaa Mkurugenzi wa EFM Majizzo na mtoto mwingine amezaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

download latest music    

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi nyingi za Diamond kufunga ndoa ambapo mwanzoni mwa mwaka huu alisema lazima ataoa lakini kwa sasa inasemekana kuwa atamuoa mpenzi wake Hamisa.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Hamisa ameweka wazi kuwa tetesi zinazoendelea kuenea kuwa yeye anaolewa na Diamond sio kweli lakini anachojua ni kwamba hana mpango wa kuzaa mtoto mwingine mpaka aolewe.

Kusema ukweli sijui kitu chochote kuhusu harusi lakini ninachojua nitazaa mtoto wangu wa tatu na mume wangu wa ndoa ambaye mpaka sasa sijui atakuwa nani”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.