“Muda wa Ali kuoa sasa umefika” Familia ya Ali Kiba wamtaka afunge ndoa na Jokate Mwegelo

Mamake na dadake Ali Kiba wametoa kauli zao kuhusu staa huyo kufunga ndoa. Wawili hao walisema muda umefika kwa Ali Kiba kuoa.

Akiongea na Global Publishers, mamake Ali Kiba alisema kuwa mwanawe anahitaji mke wa kumchungia watoto wake wanne ambao walizaliwa na wanawake tofauti.

download latest music    

“Mimi kama mzazi, ninaona muda wa Ali kuoa sasa umefika maana kama ni maisha ya ujana amesha­fanya kila kitu, ana watoto wanne na kila mmoja na mama yake, ni vi­zuri sasa akachukua mke ili aweze kuwalea hawa watoto wake. Mimi kama mzazi huu ndiyo msimamo wangu, ninamtaka ata­fakari na kuchukua uamuzi mara moja, maana ingawa siyo vizuri kwa mzazi kumpangia mtoto wake cha kufanya, lakini inapofikia suala la kuoa ni muhimu ukasimama na ku­toa msimamo, wakati wa kuoa ume­fika,” alisema mamake Ali Kiba.

Dadake Ali Kiba – Zabibu alisema kuwa Jokate Mwegelo ndo mwanamke ambaye Ali Kiba anafaa kufanga naye ndoa. Zabibu alimsifu Jokate kwa kusema kuwa ni msichana mwenye busara.

Jokate Mwegelo

“Mimi namchukulia Jokate kivingine kabisa, ni msichana mwenye busara zake na amekuwa kama mshauri wangu wa karibu mno, ningetamani angekuwa mke halali wa kaka yangu kwa sababu ana vigezo vyote vya kuwa hivyo. Kwa kuwa kaka yangu bado hajaoa, ninaomba kila kukicha na­fasi hiyo ichukuliwe na Jokate kwa sababu ni mwanamke anayestahi­li kuipata nafasi hiyo ya kuwa wifi yangu,” alisema Zabibu ambaye pia ni rafiki wa mastaa wengi,”alisema Zabibu.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere