Muigizaji wa Bongo movies – Esha Buhet alaumu ujauzito wake kwa mabaya yote anayofanya

Muigizaji Esha Buhet huyo alipata pongezi kutoka kwa mastaa wengi ilipojulikana kuwa ako na mimba, Wema Sepetu alimsifu sana Esha Buhet.

“Mashallah Esha wangu… Staha hadi Raha…. Sijawahi Elewa Wanawake wakishaenda kwenye Maternity shoots kwanini wanataka sana wakae uchi…. This Is Very Beautiful my Darling…. Allah Bariq Tumbo lako ujifungue salama my love… Unajua navyokupenda…. Hii iende kwa wanaokaaga Uchi wakiwa wanapiga picha za Mimba Jamani… @esha.s.buheti,” aliandika Wema.

download latest music    
Esha Buhet

Esha sasa amekiri kuwa mimba aliyonayo inampa kisirani ambayo imemfanya kuwakosea watu wengi bila ya yeye kusudia.

Akiongea na 3-Tamu, Esha aliwaomba watu ambao amewakosea waelewe hali aliyonayo kuwa ni ya mpito hivyo wamsamehe.

“Hali niliyonayo ni ya mpito na huwa inakuja na mambo mengi, hivyo ndugu zangu na jamaa zangu nawaomba wanisamehe sana kama ikitokea nikawaudhi maana naona mimba inanipeleka puta,” alisema Esha Buhet.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere