Muigizaji wa Bongo Zuberi Mohammed adai Wema Sepetu, Uwoya na wengine hawafikii uzuri wa mke wake

Image: Zuberi Mohammed

Mwanaume ni kujiamini na muigizaji wa Bongo Zuberi Mohammed anaejulikana kama Niva amefunguka kwa kusema kuwa mke wake anauzuri ambao Uwoya, Wema na Kajala hawana.

Wema Sepetu

Akiongea katika interview, muigizaji huyu hakuogopa kwa kuwachana warembo hawa ambao wamekuwa kwenye sekta ya burudani kwa muda sasa. Kulingana na yeye, alibarikiwa na mwanamke ambaye anauzuri ambao bado hajauona katika mwanamke mwingine.

download latest music    

“Nakuambia ukweli kabisa hakuna mwanamke mzuri Bongo Muvi zaidi ya mke wangu Maisala, wewe muamshe usingizini Uwoya, Wema, Kajala halafu muamshe na mke wangu uone nani anavutia zaidi, hakuna kama mke wangu,”

Uwoya
Uwoya

Jibu hili lake lilikuwa la kuwapasha watu ambao wamekuwa wanaosema eti anauwezo wa kumsaliti mkewe kwani kila wakati anaonekana akitembea na wasanii wa Bongo Muvi wakati alifunguka ndoa na nia ya kutulia na kuanza familia.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua