Muimbaji Wa Injili Nchini Kenya Aliyedaiwa Kubeba Mimba Ya Harmonize Afunguka

Siku mbili hizi kuna stori zilienea Kwenye mitandao ya kijamii  zilizosema kuwa Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amempachika mimba mwanadada ambaye ni msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya.

Msanii huyo anayejulikana kama Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amekataa tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote, awali Nicah alikuwa katika mahusiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke’s.

download latest music    

Tetesi hizi zimekuja mara baada ya wasanii hawa kuonekana pamoja mara kwa mara hali iliyozua minong’ono.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti moja nchini humo Veronica alisisitiza kuwa yeye sio mjamzito na hapendi kuongelea sana hayo mambo kwa sababu yeye ni Msanii wa injili hivyo si vema kuongelea.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.