Muna Amtaja Casto Kama Baba Wa Mtoto Ahaidi Kumuumbua Peter

Muigizaji wa Bongo movie na mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Muna Love amefunguka na kuweka wazi kuwa Baba wa mtoto wake Marehemu Patrick ni Casto Dickson.

Kauli hiyo imekuja baada ya utata kutanda kuhusu nani ni Baba wa mtoto baada ya mwanaume mwingine anayeitwa Peter kujitambulisha na kudai kuwa yeye ndio Baba wa mtoto.

download latest music    
Marehemu Patrick na Peter

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Muna ameweka wazi kuwa hataki utata huo anachotaka ni kumzika mtoto wake na kumtaja Casto kama Baba na msiba utakuwa nyumbani kwake Mbezi:

Jaman jamani ?????? naomba nimzike mtoto wangu ???? vaeni viatu vyangu. Kuna siri kumbwa amjawahi kuijua nawaomba nimzike mtoto wangu alafu ndiyo mnitukane. Mimi ?????? naumia jamani, namuheshimu Peter siwezi kuweka kitu hapa maana nitamwaibisha….Siwezi kumsema Casto maana yeye anajua wapi alikosea, nawaombeni jamani, naomba nataka kumzika mwanangu. Miaka miwili nahangaika na Paty wangu ????????, nimalize kumzika niongee.

Nnyiwe wanawake mnaonihumuku, vaeni viatu vya siri nilizohifadhi… baba wa mtoto ni Casto, inatosha ????????, nitukaneni mimi nife ila Paty ni kiongozi alieniongoza nione maisha mapya na nimjue Mungu… Nitalia milele mimi.

Paty wangu????????leo wanakugombania mwaanangu, natamani urudi mara moja??????????… Mwanangu ntaleta ijumaa na ntamzika Jumamosi?????, msiba uko kwangu Mbezi Beach“.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.