Muna Apewa Maono Ya Kusaidia Jamii na Marehemu Patrick

Msanii wa Bongo movie na mdau mkubwa muziki wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kutaja sababu ya yeye kujikita katika kusaidia jamii kwa sasa.

Muna amefunguka baada ya kuonekana akijikita sana katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na magonjwa ni katika kumuenzi mtoto wake aliyeaga dunia mwezi uliopita.

download latest music    

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Muna alisema kwa sasa watu wengi wamekuwa wakimuona akifanya shughuli mbalimbali za kusaidia wenye uhitaji, kazi ambayo ataifanya kwa kadiri ya uwezo wake wote kumuenzi marehemu mwanaye.

Nafanya hivi kwa sababu ni maono toka kwa Mungu, pia naona ndio njia pekee ya kumuenzi mtoto wangu kwa sababu yeye alikuwa na upendo na watoto wenziye, ilikuwa ukimpa kitu ale, hawezi kula lazima ampe na mwenziye na hata kama kipo kimoja basi yeye hatakula atampa mwenziye“.

Patrick mtoto wa Muna aliugua mwezi uliopita nchini Kenya alipoenda Kwenye matibabu baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.