Muna Awachana Wanaotaka Kujua Undani wa Maisha Yake.

Msanii wa Filamu chini, amefunguka juu ya watu wanaotaka kujua kila kitu katika maisha yake moja ya maswali hayo ni kuwa anafanya kazi gani na hela anatoa wapi? Muna kupitia ukurasa wake wa Instagram, amechapisha kuwa inatakiwa wajiulize amewezaje kupita katika moto mkali wa maumivu na kwa muda mchache yuko imara.

“Kama mwanamke unaejiamini lazima ujitambue wewe ni nani?Na unataka nini?Haijalishi umeumizwa kiasi gani na umekosa tumaini kwa ukubwa gani. Kuwa na furaha ni jukumu lako wewe mwenyewe,” amesema Muna.

download latest music    

“Hili swali kila siku mnaniuliza sijui hufanyi kazi ila unaela ?sijui mliziona wapi? unafanya biashara gani? , kila kitu mnataka kujua naomba Jambo moja ambalo mnatakiwa hasa kujua ,mjiulize nimewezaje kupita kwenye moto mkali na wamaumivu kwa Muda mchache na niko imara ?, mnazani ni mimi peke yangu ningeweza au nigejikwamua hapana , kuna mkuu kuliko wanadamu ndiyo anaenipa Jeuri na kufanya vile nyinyi mnavyoniona mpaka kuna wakati na mwambia Baba mi nakosa cha kuwajibu hawa zaidi ya kuwambia kwa Yesu kutamu.na apo Baba Ameni busti tu bado ajaachilia vya kuwashangaza ndo mtaelewa…. Njooni kwa Yesu mfurahi milele.”

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.