Muna Azungumzia Ugumu Anaoupata Kwa Kesi Ya Lulu

Mwanadada mrembo anaejihusisha na uigizaji na  mjasiriamali   Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kuongelea ugumu na kipindi kigumu anachopitia kwa kipindi hiki tangu kesi ya mdogo wake wa hiari Elizabeth Lulu Michael  imeanza.Muna Love amesema kuwa kwa kipindi hiki amekuwa na kazi kubwa  ya kuuguza mtoto wake ambae amelazwa muhimbili  kwa muda wa zaidi ya miezi miwili sasa na pia amekuwa akitakiwa kuoekana mahakamani ili kumsaidia na kumfariji mdogo wake Lulu Michael katika kesi ya mauaji inayomkabiri iliyokuwa ikisikilizwa mahakamani.

Akizungumza na Star Mix ya Global  , Muna ambae tangu kesi ya msanii mwenzie na mdogo wake huyo ianze amekuwa akonekana mahakamani bila kukosa anasema kuwa kwa takribani miezi miwili sasa amekuwa akimuuguza mwanae pale muhimbili lakini pia ana ndugu yake ambae pia anahitaji uwepo wake , hivyo inabidi aweze kufanya kotekote ingawa inakuwa inampa ugumu kidogo.

download latest music    

“Yaani najiona kabisa kama huu mwaka ni wangu,maana pale Muhimbili wameshanizoea kabisaa.Nimekaa muda mrefu nikimuuguza mwanangu mguu lakini ukiachana na mgojwa huyo pia  naangaika na upande wa pili kwa mdogo wangu Lulu mpaka nachanganyikiwa” alisema Muna Love

Kesi ya Lulu ambayo ilianza kusikilizwa mahakamani tangu Oktoba 19 inayohusu mauaji ya msanii mwenzie mkongwe ambae pia alikuwa ni mpenzi wake Steven Kanumba , iliendelea kwa muda wa takribani wiki mbili ambapo mashauri ya mwisho na hukumu yanatarajiwa kutolewa Novemba 13.Muna amekuwa ni mmoja wa watu wa karibu katika kumfariji Lulu kwa kipindi hiki kigumu ambacho anapitia na amekuwa nae bega kwa bega kila siku wanapokwenda mahakamani.

Ukiachana na wote kuwa wasanii katika tasnia moja, Lulu Michael na Muna Love wamekuwa marafiki na watu wa kakribu kama ndugu kwa muda mrefu na kusaidiana kwa mambo mbalimbali .Watu hawa wamekuwa kama ndugu sasa.

Muna pia alishawai kuwa rafiki wa karibu wa Wema Sepetu lakini mambo hayakuwa mambo na waligombana na kurushiana maneno katika mtandao wa instagram na kusababisha mahusiano yao kuvunjika

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.