Muna Kuvunja Ukimya Kufuatia Kifo Cha Patrick

Muigizaji wa Bongo movie na mdau wa Muziki wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amesema yupo tayari kufunguka kufuatia Kifo Cha Mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, amesema kwamba atazungumzia kuhusu ugonjwa wa mtoto wake, alivyoanza matibabu mpaka kifo chake pamoja na mambo mengine ambayo yalikuwa yanatokea.

download latest music    

Nisikilizwe nachotaka kuongea toka mwanangu ameumwa mpaka kufariki sikuongea kitu, Ni watu tu walikuwa wanaongea na kunihukumu, wiki ijayo nitazungumza na waandishi kuweka sawa yote”.

Wiki iliyopita Mtoto wa Muna aliyeitwa Patrick alifatiki dunia lakini gumzo kubwa lilizuka Kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari baada ya kutojulikana nani hasa Baba wa mtoto.

Wanaume wawili walijitokeza kama Baba wa watoto ambao ni Peter aliyejitambulisha kama mume wa ndoa wa Muna na Casto ambaye alikuwa anajulikana kama ndio baba wa mtoto.

Mgogoro huo ulisabisha mvutano kati ya familia ya Muna naya Peter kuhusu msiba ufanyike wapi lakini baadaye wawili hao walikubaliana msiba ufanyike kwa Peter na ndipo ratiba ya mazishi ilivyoanza mpaka malaika huyo wa Mungu kuzikwa katika makabduri ya Kinondani jijini Dar es salaam.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.